MWANAMKE AJIFANYA MJAMZITO ABEBA COCAINE KWENYE TUMBO LAKE BANDIA AKAMATWA KIAINA
Mwanamke wa Kikanada amekamatwa huko
Kolombia akiwa na madawa ya kulevya aina ya cocaine kilo mbili, mzigo
huo aliubeba katika tumbo lake bandia akijifanya mama kijacho, Maofisa
usalama walimshtukia mkanada huyo, mara baada ya kumuuliza ana mimba ya
miezi mingapi? mdada alionekana kama hakulifurahia swali hilo, baada ya
muda kidogo akajikuta akijibu kuwa, ana mimba ya miezi saba, jambo
ambalo liliwatia wasi wasi vijana 'Saidi Mwema' wa Kolombia, si ndo
wakaanza kuichunguza hiyo mimba bwana! Kugusa tumbo, tumbo gumu kama
mpira wa miguu! duuh! tumbo lenyewe bwana, likawa la baridi kama
limetolewa kwa friji, hapo ndipo msala ukaanza, tazama picha za tukio
Zima hapa chini:
Unaliona tumbo lenyewa la miezi saba!
0 maoni: